Wenje
Halima Mdee
Mbunge Zitto na Lisu
Mwishoni mwa juma lililopita uliibuka mjadala juu ya kauli za
baadhi ya viongozi wa juu wa CHADEMA kuhusiana na kufutwa uanachama kwa Mbunge
wa Kaskazini Mhe.Zitto Kabwe.
Mjadala mkubwa ulikua juu ya kauli za wabunge watatu wa CHADEMA
ambao ni Mhe.Tundu Lissu, Halima Mdee na Ezekia Wenje.
Mjadala ulianza baada ya Lissu kueleza msimamo wa Katiba juu ya
hatma ya mwanachama aliyefungua kesi mahakamani dhidi ya chama na akashindwa.
Je nini kinatokea?
KWANINI LISSU ALIKUA SAHIHI?
Lissu alieleza msimamo wa Katiba. Alichokisema Lissu si mawazo
yake. Ingekuwa mawazo yake bila shaka hata mimi ningempinga, lakini kwa kuwa ni
msimamo wa katiba huwezi kupinga unless uombe Constitutional amendment kwa
taratibu zilizowekwa.
So hata kama angesema mtu mwingine ambaye si Lissu angesema
kauli ileile aliyoisema Lissu kwamba "ukifungua kesi mahakamani dhidi ya
chama na ukashindwa unakuwa umejifukuzisha uanachama mwenyewe".
Kwa hiyo sio mawazo ya Lissu, ni msimamo wa katiba. Yani hata
angesema Mbowe, Dr.Slaa, Mnyika au mwingine yeyote angesema vilevile alivyosema
Lissu.
Wapo wanaohoji kwanini Lissu aseme na sio Mbowe ambaye ndiye
mwenyekiti? Jibu lake ni kuwa masuala ya kisheria ndani ya chama yanaweza
kusemewa na mwanasheria wa chama. Na wanasheria wa chama ni pamoja na Lissu,
John Mallya, Mabere Marando na wengineo.
Sasa nashangaa wanaohoji uhalali wa Lissu kuongelea msimamo wa
katiba ambalo ni jambo la kisheria. Mmesahau kuwa Lissu ni mwanasheria wa
Chama? Sasa kama mnajua Lissu ni mwanasheria wa chama mnashangaa nini anapotoa
ufafanuzi wa kisheria? Au mlitaka mambo ya sheria ayaongelee mlinzi wa Dr.Slaa?
KWA NINI MDEE ANAPASWA KUJIUZULU?
Halima Mdee alitweet kile alichokiita "mawazo yake"
kuwa yeye anaamini Zitto bado ni mwanachama wa CHADEMA.
Pamoja na kuwa ni mawazo yake lakini amekosea kwa kuwa yeye kama
kiongozi mkuu ndani ya CHADEMA hakupaswa kukosoa chama chake mitandaoni. Hii ni
kwa sababu anazo platform nyingi za kukikosoa chama zaidi ya mitandaoni kama
alivyofanya.
Yeye ni mjumbe wa Kamati kuu angeweza kuyasema huko. Yeye ni
M/kiti wa BAWACHA angeweza kuyasema huko, yeye ni mjumbe wa Baraza kuu la chama
angeweza kuyasema huko. Yeye ni mjumbe wa mkutano mkuu, angeweza kuyasemea
huko.
Kwa kifupi Mdee alikua na fursa nyingi za kusemea hayo mawazo
yake badala ya kusemea mitandaoni. Huku mitandaoni ni kwa wale wasio na fursa
ya kuwasilisha mawazo yao moja kwa moja kama ilivyo kwa Mdee. So katika hili
amekosea.
Pili, Mdee anajua kuwa maamuzi ya Zitto kuvuliwa uanachama ni ya
Katiba si ya mtu mmoja. Si ya Lissu wala Mbowe. Ni maamuzi ya Katiba. Na Katiba
hiyo Mdee alishiriki kuitunga mwaka 2006 akiwa Mbunge viti maalum na mjumbe wa
kamati kuu. Leo anawezaje kupinga kitu kilekile alichoshiriki kukitunga? Huu ni
wendawazimu.!
Lakini pia Mdee anajua kuwa hata kama ameona kasoro kwenye suala
hili, ni kasoro za kikatiba sio za Lissu au Mbowe. Hivyo basi mahali pazuri pa
kurekebisha kasoro hizo ni kwenye vikao vya chama si mtandaoni kama
alivyofanya. Maana hata akitweet kila siku kuwa anamtambua ZZK kuwa mwanachama,
bado Katiba iko palepale kuwa haimtambui.
Nne, Mdee ni kiongozi wa Baraza la Wanawake na alipochaguliwa
alikula kiapo cha kuilinda Katiba ya chama. Katiba aliyoapa kuilinda ndiyo
hiyohiyo inayosema "mwanachama akikipeleka chama mahakamani akashindwa
kesi amejivua uanachama wake mwenyewe."
Sasa mbona Mdee anapingana na katiba aliyoapa kuitetea na
kuilinda? Hii ni ajabu. Au alipoapa hakujua ndani kuna nini? Aliapa kuilinda
katiba asiyoijua? Lakini ataachaje kuijua na alishiriki kuitunga mwaka 2006?
This is paradox.!
Katika hili Mdee kadhalilisha nafasi yake kama Mwenyekiti wa
Baraza la wanawake na mimi nashauri AJIUZULU ili kuonesha dhana ya uwajibikaji.
Ni lazima viongozi wajifunze kuwajibika kwa kauli zao.
Hatuwezi kila siku kupigia kelele mawaziri wa serikali ya CCM
wawajibike wakati sisi wenyewe dhana ya uwajibikaji inatushinda. Kipimo
kilekile tunachowapimia CCM nasi tujipimie vivyo hivyo. Mdee achia ngazi maana
umeikana Katiba uliyoapa kuitetea.
Wengine wamehoji kwanini baada ya ile hukumu hakikukaa kikao
kikaafikiana kumfukuza Zitto badala ya Lissu tu kusema. Hawa ni wale ambao
hawajui hata wanachozungumza. Either ni watu wa vyama vingine so hawaijui
katiba ya CHADEMA au ni wapenzi wa chadema lakini hawapendi kusoma.
Sasa kwa kuwasaidia ngoja niwaambie hivi. KATIBA ya CHADEMA ya
mwaka 2006 inasema mwanachama yeyote atakayekipeleka chama mahakamani na
akashindwa anakua amejifukuzisha uanachama mwenyewe. Hii ina maana kuwa baada
tu ya hukumu kutoka automatically yeye sio mwanachama tena.
So bila haya Lissu kuongea lolote, Zitto alishajua yeye sio
mwanachama tena. Thats legal stand.
Katiba haikusema hukumu ikishatoka kamati kuu ikae itoe tamko
NO. Katiba inasema hukumu ikitoka kama umeshindwa kesi fungasha virago katafute
chama kingine.
Kwa hiyo hata kama chama kisingesema lolote. Yani Lissu angekaa
kimya na viongozi wengine wote wakakaa kimya, Zitto angeondoka tu.. maana
hakuna namna nyingine. Na ungemfuata Zitto umuulize akaamua kuwa honesty
angekuambia wazi kuwa kikatiba amejifukuza uanachama mwenyewe.
Kwa hiyo kama kuna tatizo, basi tatizo halipo kwa Lissu au
Mallya au mwanasheria yeyote wa Chadema. Kama kuna tatizo basi Tatizo lipo
kwenye Katiba ya chama.
Na ikumbukwe wakati kipengele hicho cha katiba kinaundwa mwaka
2006 Tundu Lissu hakuwa hata mwanachama wa CHADEMA (alikua Nccr Mageuzi), so
huwezi kuhoji legitimacy yake kwenye hicho kipengele.
Labda ambaye anaweza kuhojiwa kwanini kipengele hicho kiliwekwa
na akatoa maelezo mazuri ni Mhe.Zitto Kabwe ambaye wakati marekebisho ya katiba
yanafanyika mwaka 2006 yeye alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu.
Kwa hiyo yeye ndiye anayeweza kutupa logic ya hicho kipengele.
Walikiweka ili iweje? Walimlenga nani? Kama alishiriki kuweka kipengele hicho
mbona analalamika kinapotumika kwake? Alitaka kitumike kwa nani?
Ikumbukwe sheria ni msumeno hukata huku na huku. Unapotunga
sheria yoyote jiulize hii sheria ikitumika kwangu nitajisikiaje? Sio unatunga
then ikikurudia unahisi umeonewa.
Viongozi wengi wa kiafrika wanapotunga sheria kandamizi
(Draconian Laws) hudhani ni kwa ajili ya tabaka la chini tu na sio kwa ajili
yao. Siku zikiwageuka wanaanza kutafuta mchawi. Katika hili Zitto hapaswi
kulalamika kabisa kuhusu kifungu cha katiba kinachomvua uanachwma maana
alishiriki kukitunga mwaka 2006.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni