Tuliwahi kuandika stori ya mwanamke kujifungua watoto mapacha ambao walipishana miezi miwili waliozaliwa katika moja ya hospitali huko Romania na kuonekana kugusa hisia za watu wengi.
Sarah Ward mwenye umri wa miaka 29 alipata mapacha watatu ikiwa ni mwezi mmoja tangu ajifungue mtoto wake wa kwanza wa kiume,
Mwanamke huyo alijifungua mapacha hao watatu ambao walizaliwa kabla ya muda huku mtoto wake wa kwanza akiwa tayari na miezi nane.
Sarah amesema anashukuru kupata watoto hao na amekua akitumia nepi zaidi ya 30 kwa siku kwa ajili ya kuwabadilisha watoto wake lakini haoni kama ni gharama kutokana na furaha aliyonayo.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni