Jumatatu, 23 Machi 2015

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AMJULIA HALI MZEE ISRAELI NAWINGA KIJIJINI KWAKE MASAMA LOSAA WILAYANI HAI.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akipeana mkono na Bwa.Israel Elly Nawinga mapema leo asubuhi katika kijiji cha Masama Losaa,Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro,Pichani kulia ni Mkuu mpya wa Wilaya ya Hai,Mh Anthony Mtaka.Bwa.Israel aliwahi kuwa Waziri wa Elimu na pia Waziri wa Mambo ya Nje kwa nyakati tofauti enzi za uongozi wa Mwal.Julius Kambarage Nyerere.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wapo mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya siku tisa ya kukagua,kuhimiza na kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya chama cha CCM ya mwaka 2010 ikiwemo pia kusikiliza matatizo ya wananchi na kuyatafutia ufumbuzi
Bwa.Israel Elly Nawinga akiuzungumza jambo na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana mapema leo asubuhi alipopita kumsabahi katika kijiji cha Masama Losaa,Wilaya ya Hai mkoani KilimanjaroBwa.Israel aliwahi kuwa Waziri wa Elimu na pia Waziri wa Mambo ya Nje kwa nyakati tofauti enzi za uongozi wa Mwal.Julius Kambarage Nyerere.

PICHA NA MICHUZI JR-HAI  MKOANI KILIMANJARO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni