Alhamisi, 19 Machi 2015

JENNIFER MGENDI AACHIA ALBAMU YA WEMA NI AKIBA


 Mwimbaji wa siku nyingi wa nyimbo za injili nchini, Jennifer Mgendi, 
ameachia albamu yake mpya mapema wiki hii.

Akizungumza na blogu hii  Mgendi amesema albamu hiyo ina jumla ya nyimbo saba ambazo ni Wema ni Akiba, Nani kama Mungu?, Nakungoja aliomshirikisha Mchungaji Abiudi Misholi, Kimbilia Msalabani, Nakuhitaji Roho, Tenda nishangae na Wastahili.

Akizungumzia video ya albamu hiyo, Mgendi amesema maandalizi ya video yameanza na video itazinduliwa Juni 28 katika kanisa la DCT Tabata Shule katika tamasha litakaloambatana na shukurani ya kutimiza miaka 20 tangu aanze uimbaji. 

Mbali na uimbaji Jennifer pia ni muandaaji wa filamu mbalimbali za kidini hadi sasa akiwa na filamu tano Joto la roho, Pigo la faraja, Teke la Mama, Chaimoto na Mama Mkwe.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni