Jumatatu, 23 Machi 2015

FEROUZ KUTOKA UPYA NA MKUBWA NA WANAE

SHARE THIS
TAGS
FerouzNA MWANDISHI WETU
BAADA ya kimya kirefu, msanii Ferouz anatarajiwa kutoa wimbo mpya katika mahadhi tofauti na mchiriku.
Meneja wa kundi hilo la Mkubwa na Wanae, Chambuso, amesema kwamba ameamua kumrudisha upya msanii huyo baada ya kufanya hivyo katika wimbo wake wa mchiriku na kisha kuwa kimya kwa muda.
“Mwanzo tulimtoa katika wimbo wa mchiriku halafu akawa kimya kwa muda lakini sasa tunamtoa upya tena na anakuja kwa staili yake ya awali aliyokuwa nayo, tangu alipokuwa katika kundi la Daz Nundaz,’’ alisema meneja huyo.
Aliongeza kwamba huo ni utaratibu uliowekwa na uongozi wa kundi hilo ambalo lina idadi kubwa ya wasanii na wengi wao bado hawajapata nafasi ya kusikika.
“Wasanii wapo wengi katika kundi letu lakini kwa sasa tunamrudisha upya Ferouz na wasanii wengine wengi, huku tukiandaa mradi wetu wa wasanii wa nyimbo za mchiriku kama alivyokuwa Ferouz na hivi karibuni tutaweka wazi kazi zao,’’ alisema Chambuso.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni