Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya kulia akihutubia katika maadhimisho ya siku ya sheria nchini Mkoni Rukwa leo tarehe 04/02/2015 katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga. Kaulimbiu ya maaadhimisho hayo ikiwa "Fursa ya kupata haki: Wajibu wa Serikali, Mahakama na Wadau". Katika hotuba yake hiyo alisema ipo haja kubwa kwa Serikali kubadili sheria zake ili lugha ya mahakamani na hukumu ziandikwe kwa kiswahili. Kwa upande wa wananchi aliwaasa kujiepusha na tabia ya kujichukulia sheria mkononi ili kudumisha amani nchini.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Mhe. Jaji Sambo akipokea gwaride la heshima kutoka kwa kikosi cha Jeshi la Polisi wakati wa maadhimisho ya siku ya Sheria Mkoani Rukwa leo tarehe 04/02/2015.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Mhe. Jaji Sambo katikati akisoma hotuba yake ya maadhimisho ya siku ya sheria Mkoani Rukwa ambapo aliwataka mahakimu wote Mkoani Rukwa kutimiza majukumu yao ipasavyo kwa mujibu miongozo ya mahakama ili kusaidia uharakishwaji wa utoaji haki kwa wananchi kwa wakati. Aliwaeleza pia wadau wote wa sheria wakiwepo mawakili wa kujitegemea kuwa mashauri yote ya kesi yatakua yakisimamiwa na kutolewa maamuzi na mahakama na sio mawakili kutaka kuingilia utendaji wa mahakama.
Baadhi ya wadau na viongozi wa Sheria na Serikali katika meza kuu.
Sehemu ya mahakimu, mawakili, wanasheria na wageni waalikwa katika maadhimisho hayo.(Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa@rukwareview.blogspot.com)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni