Kwenye 255 ya leo Feb 5, kuna story za wasanii Malaika, Cyril na Muigizaji Rose Ndauka..
Nakukaribisha kwenye 255 ya leo na story ya kwanza amesikika msanii Malaika ambae alizindua video ya wimbo wake unayoitwa ‘Mwantumu’ hivi karibuni, amezungumzia kuhusu collabo ambazo amewahi kuzifanya ikiwemo ya msanii Chege (Uswazi Take Away), Ney wa Mitego na ipo ya msanii mwingine ambae hawezi kumtaja kwa kuwa wimbo waliofanya bado haijatoka.
Msanii Cyril amepiga story na 255 na kuzungumzia kuhusu ishu ya kuwasaidia watoto watatu ambao alikutana nao katika mizunguko yake ya kazi na baada ya kuzungumza nao aligundua kuwa hawasomi, akaguswa kuwasaidia na baada ya kuzungumza na wazazi wao, aliwatafutia shule na kuwalipia ada wakaanza masomo.
Muigizaji Rose Ndauka amefungua Online Magazine inayoitwa Rose Magazine kwa lengo la kurahisisha mashabiki zake kupata kazi zake kwa wakati na pia wasanii wengine wapate nafasi ya kutangaza kazi zao kw kuwa ni Magazine inayohusu mastaa wote na watu wengine wanaofanya vitu mbalimbali kwenye jamii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni