Baby Madaha atamani mtoto
MWIGIZAJI na msanii wa Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha, amesema anatamani kuitwa mama kama ilivyo kwa wanawake wengine wenye watoto. Akizungumza na MTANZANIA jana, Baby Madaha, alisema amepanga kufanikisha ndoto zake za kuwa mama mwaka huu. “Kiukweli natamani sana kupata mtoto, nafarijika nikisikia na kuona wenzangu wanaitwa mama, ni jambo la busara na kumuomba Mungu ili litimie,” alisema Baby Madaha. Madaha alisema wasanii wengi wamefululiza kuzaa jambo ambalo linapendeza katika jamii, lakini uamuzi wake si wakufuata mkumbo kama ambavyo wengi watafikiria.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni