Jumanne, 23 Desemba 2014

MSD YAKUBALI AGIZO LA SERIKALI KUWEKA ALAMA KATIKA DAWA NA VIFAA TIBA

NA CHALILA KIBUDA GLOBU YA JAMII,DAR

KAIMU Mkurugenzi  Mkuu wa Bohari ya Dawa nchini (MSD),Cosmas Mwaifwani amesema bohari ya dawa imepokea agizo la serikali kuweka alama katika dawa  za umma pamoja na vifaa tiba ili kuweza kudhibiti upotevu wa dawa pamoja na vifaa tiba.

Mwaifwani aliyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya mikakati  bohari hiyo katika kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.

Alisema katika mkakati mwingine ni kuanzisha maduka ya jumla ya dawa na vifaa tiba ikiwa ni lengo ya kuweza kusambaza  dawa katika ngazi zote kuliko ile ya dawa kufika katika ngazi za wilaya.


“Ifikapo Januari 30  mwakani ,MSD itatekeleza mabadiliko yenye lengo la kuhakikisha dhima ya kuwezesha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba vyenye ubora na bei nafuu ambayo kila mtanzania anaweza kumudu hiyo na utekelezaji huo ni vitendo na sio kusema bila kufanya utetekelezaji”alisema Mwaifwani.


 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa nchini (MSD),Cosmas Mwaifwani akizungumza na waandishi wa habari( hawapo pichani) kuhusu mradi wa uzalishaji dawa na Vifaa tiba kwa Ubia wa sekta Binafsi katika ukumbi wa idara ya habari Maelezo jijini Dar es Salaam.


Waandishi wa habari wakichukua habari ya kaimu Mkurugenzi wa MSD. 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni