Rasi Jakaya Kikwete akipokea zawadi ya saa kutoka kwa Robert Shumake, ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya M/S Shumoja inayotajwa kuwa itawekeza katika mradi wa usafiri wa treni ya kisasa Dar
SERIKALI
imetia saini mkataba wa uwekezaji wa pamoja kati yake na kampuni ya Marekani
kwa ajili ya kuanza mradi wa usafiri wa treni ya kisasa itakayoanzia Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere (JNIA) hadi katikati ya Jiji la Dar es
Salaam.
Waziri
wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amesisitiza ni lazima kufanya haraka kwani
mwekezaji, Kampuni ya Ms Shimoja ya Marekani, iko tayari hata sasa kuleta treni
hizo aina ya Diesel Multiple Unit (DMU) ambazo ni za kisasa, itakayopita kila
baada ya nusu saa.
Usafiri
huo wa treni kwenye njia ya umbali wa kilometa 13 kutoka uwanja wa ndege hadi
katikati ya jiji, unatarajiwa kukamilika Desemba mwaka huu au mapema mwakani
ukilenga kubeba abiria kati ya 800 na 1,000.
Katika
hafla ya kutia saini kati ya mwekezaji huyo na Shirika la Reli Tanzania (TRL)
jana jijini Dar es Salaam, Waziri Mwakyembe aliwaambia watendaji kwamba ikiwa
watafanya haraka, baada ya wiki mbili watasaini makubaliano ya mwisho na kuanza
urekebishaji na ujenzi wa vituo sita vya kupandia treni kwa kadi.
Mkurugenzi
wa Kampuni hiyo ya Ms Shimoja, Dk Robert Shumake na Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,
Kipallo Kisamfu walitia saini jana katika hafla iliyoshuhudiwa na Waziri
Mwakyembe na Katibu Mkuu wake, Dk Shaaban Mwinjaka.
Waziri
Mwakyembe alimshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kusafisha njia ya kupata
wawekezaji, akiwemo mfanyabiashara huyo mkubwa ambaye ametajwa kuwa na imani
kuwekeza katika mradi huo utakaogharimu zaidi ya dola za Marekani milioni 35.
Kwa
mujibu wa waziri, waliamua kuanza mradi huo baada ya kuhamasisha mashirika
makubwa ya ndege kufanya safari katika kiwanja hicho cha ndege. Hata hivyo,
alisema wasafiri wanapata kero ya usafiri kufika katikati ya jiji jambo
wanalotegemea mradi kuondoa kero hiyo.
“Mabehewa
hayo yataunganishwa kulingana na idadi ya abiria waliopo na muda, huku
mwekezaji akiwekeza bila masharti kama walivyo wengine; kama vile kutaka
dhamana ya serikali,” alisema Mwakyembe.
Hata
hivyo alisisitiza, “lakini ni lazima watendaji waache ukiritimba kwa kufanya
utaratibu haraka ili kazi zianze.”
Alisema
katika utaratibu wa PPP, uwekezaji na idara nyingine lazima wafanye haraka.
Aidha alitaka watendaji TRL kumsihi mfanyabiashara huyo kuleta treni nyingine
mbili za Ubungo mpaka Stesheni na kwingineko.
Treni
hiyo itasaidia kupunguza adha kwa abiria wanaosafiri kwa ndege, ambapo katika
kituo cha Karakata, itajengwa njia ndogo ya treni mpaka barabarani. Pia
litajengwa daraja kwa ajili ya wasafiri kuvuka na mizigo yao.
Akizungumza
katika hafla hiyo ya utiaji saini, Mkurugenzi Mtendaji wa TRL, Kisamfu alisema
watafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha usafiri huo unaanza mapema
iwezekanvyo kutoka katikati ya jiji hadi Pugu kupitia maeneo ya Karakata,
kwenye Uwanja wa Ndege kwa kutumia Reli ya Kati.
Mwekezaji
Dk Shumake ambaye ni Balozi wa Heshima Tanzania nchini Marekani, alisema wako
tayari kuanza mradi huo hata leo kama utaratibu utakamilika.
Alisisitiza kwamba uwekezaji huo utaondoa tatizo la foleni barabarani
kutoka uwanja huo wa kimataifa wa ndege hadi katikati ya jiji.
CHANZO: Habari Leo |
Jumanne, 7 Oktoba 2014
UCHAMBUZI: MRADI WA TRENI YA KISASA DAR: KUPUNGUZA KERO YA USAFIRI AU CHANGA LA MACHO KAMA RICHMOND?
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni