Mshambuliaji wa kilabu ya Liverpool Mario Baloteli hutumia pauni 500 kila wiki ambazo ni sawa na Sh72,000 (£500) kila wiki kujitengeza nywele.
Inadaiwa kuwa mchezaji huyo ambaye hupendelea kunyoa mtindo wa Mo Hawk mbali na kubadilisha rangi ya nywele zake humlipa kinyozi wake ili kumtembelea nyumbani kwake mara tano kwa wiki.
Duru zimeliambia gazeti la the Sun nchini Uingereza kwamba Mario huwa mkarimu sana na hulipa pauni hamsini sawa na shilingi 7200 fedha sa kenya kila anaponyolewa.
''Ijapokuwa fedha hizo zinaonekana kuwa nyingi yeye hupendelea kunyolewa kila siku ili kuimarisha mtindo wake wa nywele''.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni