Jumatano, 29 Oktoba 2014

FIFA:Nigeria yakabiliwa na marufuku

NFF
Nigeria inakabiliwa na marufuku ambayo huenda ikaitupa nje kushiriki katika michuano ya taifa bora barani afrika mwaka ujao.
Hii ni kufuatia uamuzi wa mahakama kuu kuhusu matokeo ya uchaguzi katika shirikisho la soka nchini humo.
Mahakama kuu ya Jos ilifutilia mbali uchanguzi wa Amaju Pinnick kama Rais wa Shirikisho la kandanda Nigeria
Hii ni mara ya pili Nigieria kupigwa marufuku kwa sababu ya serikali kuingilia masuala ya shirikisho hilo.
Shirikisho la soka duniani FIFA limetoa onyo kuwa kuingiliwa kwa maswala ya kandanda kutasababisha Nigeria kupigwa marufuku hadi May 2015
Hatua hiyo inaamanisha kuwa Nigeria watapoteza nafasi yao ya kushiriki katika michuano hiyo mwaka 2015 iwapo
Rais wa shirikisho la kandanda Afrika (Caf) Issa Hayatou amekutana na viongozi wa shirikisho la kandanda la Nigeira mjini Windhoek, Namibia baada ya kukamilika kwa fainali za kombe la bara afrika miongoni mwa akina dada.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni