Jumatatu, 6 Oktoba 2014

CCM IRINGA CHAWASHANGAA CHADEMA KUZUIA WANACHAMA WAKE KUNYWA MAZIWA

Bw.Hassan Mtenga  

CHAMA  cha mapinduzi (CCM) mkoa  wa Iringa chakishangaa chama cha demokrasia na maendeo (CHADEMA) kwa  kuwazuia  wanachama  wake  mjini Iringa  kunywa maziwa  ya  Asas Dairies Ltd
 
Akizungumza na  waandishi  wa habari  ofisini  kwake jana katibu  wa  CCM  mkoa  wa Iringa  Hassan Mtenga  alisema  kuwa  hatua ya  Chadema  kuwazuia  wanachama  wake  mjini  Iringa kunywa maziwa ni dalili  mbaya kwa  mbunge  wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa mwaka 2015.

Kwani  alisema kuwa kuwazuia  wanachama  wao kunywa maziwa ni moja ya hatua ya  kuwataka kufa kabla  ya  uchaguzi  mkuu mwaka 2015  kwani maziwa ni tiba tosha kwa watu  wenye matatizo na  wasio na matatizo.

Mtenga  alisema  kuwa maziwa  ya  Asas Dairies Ltd hayana  uhusiano  wowote na chama chochote  cha  siasa  na  kuwa  hatua ya   viongozi  wa chadema kuacha kuzungumzia kazi  ambazo mbunge  wao  Msigwa  amefanya na  kuelekeza mapambano yake  katika maziwa  si  siasa  bali ni  kuishiwa hoja  za kuwaeleza wananchi.

“Tunashangazwa   sana na  uwezo  wa uelewa wa viongozi  wa Chadema hivi kweli  inaingia akilini kiongozi ama  chama  kumzuia mwanachama  wake  kunywa maziwa ama kula ? kweli  ni  kufirisika  kisera maana  bila mtu kula  atakufa na nani atakupigia  kura ” alihoji Mtenga.
 
Hata  hivyo  alisema  kuwa  hakuna  asiyetambua  kuwa wapo  wafanyabiashara  ambao ni wanachama wa  Chadema   kama hivyo ndivyo basi  CCM kuwatangazia  wanachama  wake  kuwa wasinunue wala kuingia  katika maduka ama kupenda  bidhaa za wafanyabiashara  ambao  ni  wanachama wa Chadema nchini.
Alisema  kuwa kuwa kawaida  chama  kina mpaka yako katika  kuwaongoza wananachi na wananachi  ama  wanachama  wana uhuru  wa  kupenda chochote  bila kuvunga  sheria .

Hivyo  alisema kuwa  chadema  wanapaswa kuwaomba radhi  wananchi  wa  jimbo la Iringa kwa kauli hiyo ambayo ni sawa na  kumzuia mtu  kula ama  kuishi vinginevyo CCM kinawataka  wananchi kupuuza kauli  hiyo ambayo  imelenga  kuwaondolea haki ya kuishi.

Pia  alisema  iwapo wanachama  wana biashara  zao si vema vyama kuhusisha biashara  ya  mtu na itikadi  za vyama na  kudai kuwa  viongozi wa chama wapo kwa ajili ya kuvuruga biashara  za  watu .
CCM kimetoa kauli  baada ya  viongozi wa chadema Iringa  mjini na makamu  mwenyekiti wa baraza la vijana Taifa (BAVICHA ) Patrick Sosopi kutumia mkutano wake  wa hadhara  kuwazuia  wananchi  kunywa maziwa hayo ya asas kwa  kudai  kuwa mmoja kati ya  wanafamilia  wa mmiliki  wa kampuni  hiyo anasaidia CCM Iringa .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni